Mlipuko watokea huko Houston nchini Marekani

2 wapoteza maisha na wengine 18 wajeruhiwa kufuatia mlipuko huo

Mlipuko watokea huko Houston nchini Marekani

Watu 2 wamefariki huku wengine 20 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika eneo moja la viwanda kwenye jimbo la Texas nchini Marekani.

Meya wa Houston, Sylvester Turner alisema pindi mlipuko ulipotokea wafanyakazi 2 wa kiwanda, Frank Flores na Gerardo Castorena ambao walikuwa nje ya masaa yao ya kazi walikuwamo katika jengo hilo wakitumia eneo la mazoezi kwa ajili ya wafanyakazi.

Turner alisema kwamba Flores na Castorena walipoteza maisha katika mlipuko huo, watu weigne 18 walikokuwa katika nyumba zinazozunguka eneo la tukio walipata majeraha.

 Habari Zinazohusiana