Juhudi za Uturuki na Urusi nchini Libya zazaa matunda

Mapigano yasitishwa, wananchi wa Tripoli washangilia kwa vifijo na fataki

Juhudi za Uturuki na Urusi nchini Libya zazaa matunda

Wito wa Uturuki na Urusi wa “kusimamisha mapigano” nchini Libya wazaa matunda.

Majeshi ya Khalifa Haftar kiongozi wa uasi mashariki mwa Libya yamekubali kusimamisha mapigano.

Mapigano hayo yalisimama muda wa saa 00.00 mnamo tar 12/01 kwa masaa ya eneo hilo.

Msemaji wa majeshi ya Hafter, Ahmed al Mismari kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii aliandika, “tumekubali wito wa kusitisha mapigano magharibi mwa Libya lakini ikitokea upande wa pili wakakiuka kusimamisha mapigano tutajibu mapigo vikali mno”

Kusimamishwa kwa mapigano kulipokewa vizuri mji mkuu Tripoli, kwa shangwe za fataki.Habari Zinazohusiana