Kisanduku cheusi cha ndege ya abiria Ukraine iliyodunguliwa kutumwa Ufaransa

Iran imeridhia kisanduku cheusi cha ndege ya abiria ya Ukraine iliyodunguliwa kimakosa nchini humo kwenda kuchunguzwa nchini Ufaransa

Kisanduku cheusi cha ndege ya abiria Ukraine iliyodunguliwa kutumwa Ufaransa

Iran imetangaza imechukua uamuzi wa kupeleka Ufaransa kwa uchunguzi zaidi kisanduku cheusi che ndege ya abiria ya Ukraine iliyodunguliwa “kimakosa” na mfumo wa ulinzi wa anga wa nchi hiyo.

Akizungumza na shirika la rasmi la habari la Iran, IRNA  mkurugenzi wa ofisi ya ajali katika shirika la urubani na ndege za kiraia, Hasan Rizayifer alisema Iran haina uwezo wa kutosha kuweza kusoma kumbukumbu zilizo katika kisanduku cheusi cha ndege.

“Tumetuma maombi kwa Canada. Ufaransa na Marekani watutumie program tumizi na vifaa vya kutuwezesha kusoma kumbukumbu za kisanduku cheusi cha ndege hiyo, lakini nchi hizo zimekataa maombi yetu”.

Rızayifer alifahamisha kwamba mwishoni waliridhia  kisanduku cheusi kiende maabara za nchini Ufaransa kwa uchunguzi zaidi na kusomwa kumbukumbu zilizorekodiwa.Habari Zinazohusiana