Moyo wa bandia uliotengenezwa nchini Uturuki watambulishwa nchini Marekani

Madaktari zaidi ya 20 kutoka Uturuki wametambulisha moyo bandia Uliotengenezwa nchini Uturuki katika maonyesho makubwa ya Veith Sempozium yaliyofanyika jijini New York, Marekani

Moyo wa bandia uliotengenezwa nchini Uturuki watambulishwa nchini Marekani

Kifaa cha moyo wa bandia uliotengenezwa Uturuki kimetambulishwa nchini Marekani katika maonyesho makubwa ya Veith Sempozium.

Madaktari zaidi ya 20 kutoka Uturuki walifanya kazi ya kutambulisha kifaa hicho.

Vifaa tiba chapa ''Invamed na RD Global''  vilivyobuniwa na wanasayansi wa Uturuki  vilitambulishwa katika maonyesho makubwa duniani ya Veith Sempozium msimu wa 46. Zaisi ya mashirika 70 kutoka nchi mbalimbali duniani yalishiki maonyesho hayo. Maonyesho hayo pia yalipata wahudhiaji takribani elfu 4 na 500.

Rais wa baraza la Afya la Uturuki Raşit Dinç, alipokuwa akitambulisha vifaa tiba kutoka Uturuki alisema

“Nchini Uturuki kila uchwao yanafanyika mambo mazuri zaidi. Hivi sasa dunia inazungumzia juu ya kifaa cha moyo bandia kinachotumika wakati wa upasuaji 'Turkish glue' pamoja na maroboti ya mishipa ya damu vyote vimebuniwa na kutengenezwa Uturuki.”

Dinc alikumubushia kwamba Maroboti ya mishipa huweza kuingia na kuzibua mishipa ya damu iliyoziba pamoja na vifaa vingine vya kuondoa donge la damu linaloweza kuziba mishipa ya ubongo, vifaa hivyo vyote vinatengenezwa nchini Uturuki.

'Hivi sasa vifaa tiba vinavyotengenezwa nchini Uturuki huuzwa zaidi ya mataifa 60 duniani.

Mwakani tunatarajia kuuza vifaa hivyo nchini Marekani pia, Kupitia maonyesho haya tumetambulisha vifaa vyetu kwa zaidi ya mataifa 100, vifaa vya upasuaji wa mishipa ya damu vimeonyesha kuwavutia sana wahuzuriaji”.

 Habari Zinazohusiana