Umoja wa Ulaya watolea wito mitandao ya kijamii kuhusiana na habari za uongo

Umoja wa Ulaya umeitaka mitandao ya kijamii kuchukua tahadhari stahiki kuzuia kusambazwa kwa habari za uongo na uwepo wa akaunti bandia

1188632
Umoja wa Ulaya watolea wito mitandao ya kijamii kuhusiana na habari za uongo

Umoja wa Ulaya umetolea wito mitandao ya kijamii ya Twitter, Facebook na Google kuongeza juhudi katika  kupiga vita habari za uongo.

Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imetoa taarifa ya mwezi  inayofanya tathmini kuhusu habari za uongo zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

Katika taarifa hiyo imesifu kazi iliyofanywa na mitandao ya Twitter, Facebook na Google katika kuongeza uwazi kabla ya uchaguzi wa bunge la Ulaya.

Ripoti hiyo ilisema kitendo cha mitandao ya kijamii kutoa ishara kwa matangazo ya kisiasa  ni hatua chanya na kwamba nguvu zaidi inabidi iwekwe katika kupiga vita habari za uongo na akaunti bandia.

Umoja wa Ulaya umeitaka mitandao ya kijamii kuchukua tahadhari stahiki kuhakikisha inazuia matatizo yasitokee katika uchaguzi wa bunge la Ulaya utakaofanyika mwezi Mei.

 Habari Zinazohusiana