Leo katika Historia

Leo katika Historia

Leo katika Historia

Karibu mpenzi mskilizaj wa vipindi vyetu Idhaa ya kiswahili Sauti ya Uturuki.
Kipindi chetu Leo Katika Historia huwa tukiwaletea matukio muhimu yaliotokea katika Historia.
Aprili 16 mwaka 1912,  Harriet Quimby alikuwa mwanamke wa kwanza rubani Marekani kurusha ndege Mansh.  Rubani huyo alifariki meizi  mitatu  baadae katika jali iliotokea  ya ndege akiwa rubani katika maonesho.

Aprili 16 mwaka 1941,  zaidi ya ndege 500 za jeshi la Ujerumani zilishambulia  usiku kucha jiji la London .  Katika vita hivyo Ujerumani  ilishambulia "The Blitz" Uingereza. Oktoba  mwaka 1940 hadi Juni  mwaka 1941 watu zaidi ya 32000 waliuawa na wengine wasiopngua 87 000 walijeruhiwa.

Aprili 16 mwaka 1945,  Jeshi la Urusi lilivamia jiji la Berlin na vita vya Berlin kuanza.
Aprili  16 mwaka 1948 kuliundwa  muungano wa  ushirikiano wa kiuchumi Ulaya. Mataifa tajiri na yalioendelea 36 ni wahsirika katika muungano huo.
Aprili 16 mwaka 1972,  safari katşa anga za mbali na kifaa cha Apollo 16 ilianza.
Aprili 16 mwaka  2017 Uturuki iliingia katika mfumo wa uongozi wa urais.Habari Zinazohusiana