Sarkozy alipokea dola milioni 8 kutoka kwa Gaddafi

Rais wa zamani wa Ufaransa alipokea msaada wa dola milioni 8 kutoka kwa kiongozi wa mapinduzi ya Libya Muammar Gaddafi

Sarkozy alipokea dola milioni 8 kutoka kwa Gaddafi

Mkuu wa Intelijensia wa kiongozi wa mapinduzi ya Libya Abdullah es-Sennusi, amesema rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarcozy alipokea kutokea kwa Muammar Gaddafi dola milioni 8 kwa ajili ya kufadhili kampeni zake za uchaguzi. 

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na ukurasa wa mtandao wa habari wa Ufaransa, Mediapart, Mahakimu wa Ufaransa walimhoji mkuu wa Intelijensia wa Gaddafi ambaye pia alikuwa ni shemeji yake,Abdullah es-Sennusi.

Katika mahojiano hayo Sennusi aliwaambia mahakimu hao Gaddafi alimpatia msaada wa dola milioni 8 Sarkozy kwa ajili ya kampeni, Na yeye binafsi ndiye aliyeratibu utumwaji wa fedha hiyo kwenda kwa Sarkozy.

Sarkozy kulipa fadhila ya msaada huo alitakiwa airekebishe taswira ya Gaddafi kimataifa. Ahakikishe kesi dhidi ya Gaddafi na wasaidizi wake zinafutwa pamoja na kusimamisha amri iliyokuwako ya kumkamata Gaddafi.

 Habari Zinazohusiana