Rais Erdoğan amtaka rais Macron kusoma kwanza Historia

Rais wa Uturuki amtolea wito wa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kusoma kwanza Historia kabla ya kutumia kimakosa mtukio ya mwaka 1915

Rais Erdoğan amtaka rais Macron kusoma kwanza Historia

Rais wa Uturuki amtolea wito wa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kusoma kwanza Historia kabla ya kutumia kimakosa mtukio ya mwaka  1915

Recep Tayyıp Erdoğan rais wa Uturuki amtolea wito rais wa  Ufaransa kujifunza kwanza Historia kabla ya kutumia kimakosa  matukio ya mwaka 1915.

Rais Erdoğan amemtolea wito Macron kujifunza kwanza historia ya taifa lake na ukiukwaji wa haki za binadamu iliotenda katika mataifa  tofauti barani Afrika.

Katika mahojianao aliofanya na waandishi wa habari, rais Erdoğan amesema kuwa Marekani inaweza kuonesha ushirikiano wake  na Uturuki kwa kumrejesha kiongozi wa kundi  la FETÖ, kundi ambalo  bila shaka  ndilo lililohusika na jaribio la mapinduzi Uturuki kwa mujibu wa serikali ya Uturuki.

Rais Erdoğan amekemea  Marekani kwa kumpa hifadhi kiongoni wa kundi la FETÖ aliendesha jaribio la mapinduzi Julai 15 mwaka 2016.

Uturuki kwa ushirikiano na wizara yake ya sheria imetuma nyaraka zaidi ya 85 Marekani ambazo zinaweka wazi kundi la FETÖ kuhusika na jaribio la mapinduzi Uturuki.

Katika mahojiano hayo , rais Erdoğan amezungumzia pia kuhusu tamko la rais wa Marekani Donald Trump linasubiriwa kwa kusema kwamba bila shaka ni kuhusu ushindi dhidi ya kundi wa wanamgambo wa Daesh.

Kuhusu matukio ya mwaka 1915, rais Erdoğan amesema kuwa waarmenia zaidi ya laki moja ni raia wa Uturuki na kumtaka rais Macron kusoma historia ya taifa lake barani Afrika.

Kwa kumalizia, rais Erdoğan amaekumbusha wito wake kuhusu uchunguzi wa kimataifa kuhusu mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi alieuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia  mjini Istanbul.Habari Zinazohusiana