Ndege ya jeshi yaanguka na kusababisha vifo vya watu wawili Vietnam

Watu wawili wamepoteza maisha baada ya ndege ya jeshi kuanguka Vietnam.

1021197
Ndege ya jeshi yaanguka na kusababisha vifo vya watu wawili Vietnam

Watu wawili wamepoteza maisha baada ya ndege ya jeshi kuanguka Vietnam.

Rubani na msaidizi wake wamepoteza maisha muda mchache baada ya ndege hiyo kuanguka wakati ikitoka katika uwanja wa ndege wa Sao Vang.

Sababu ya ajali hiyo imetabiriwa kuwa ni mvua ambazo zimeendelea kunyesha kwa muda nchini humo.

Uchunguzi zaidi wa chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo unaendelea.

Mnamo mwaka 2016,ndege nne za kijeshi zilianguka na kusababisha vifo vya watu 14 nchini humo.Habari Zinazohusiana