Maandamano yapamba moto Iraq

Serikali nchini Iraq imefanya mkutano wa dharura baada ya maandamano kufika katika mji mkuu wa Baghdad.

Maandamano yapamba moto Iraq

Serikali nchini Iraq imefanya mkutano wa dharura baada ya maandamano kufika katika mji mkuu wa Baghdad.

Maandamano hayo yamefanywa dhidi ya ukosefu wa ajira na vilevile uhaba wa huduma muhimu nchini humo.

Mamlaka nchini humo yamelazimika kukata internet.

Kwa mujibu wa habari,maandamano hayo yaliyoanza mjini Basra siku ya Ijumaa sasa yanaelekea mjini Baghdad.

Waandamanji wamewataka baadhi ya maafisa wa serikali kujiuzulu haraka iwezekanavyo.

Maafisa usalama wamekuwa wakijaribu kuyatuliza maandamano hayo bila mafanikio.

 Habari Zinazohusiana