Kurejeleza

Kurejeleza ni nini? Ni vitu vipi tunavyoweza kurejeleza?

278386
Kurejeleza

Bidhaa nyingi tunayotumia hutengenezwa kwa kutumia malighafi inayotolewa kutoka kwa vyanzo vya asili. Jinsi idadi ya watu inavyoendelea kuongezeka matumizi ya bidhaa hii pia inaendelea kuongezeka. Jambo hili linapelekea kupungua na hata kumalizika kwa vyanzo hivi. Ili kuweza kulinda vyanzo hivi vya asili hatuna budi kuvumbua mbinu mpya na mwafaka ya kutengeneza bidhaa hii. Miongoni mwa mbinu zilizovumbuliwa katika jitihada za kulinda vyanzo vya mali asili ni falsafa ya kurejeleza.

Kurejeleza ni mbinu ya kutibu taka ambayo kwa kawaida ingekuwa haiwezi kutumika kupitia utaratibu wa kemikali au kusagwa kwa mashine. Baada ya kupitia utaratibu huu taka hiyo hubadilishwa na kuwa katika hali ambayo inaweza kutumika kama malighafi ya kutengezea bidhaa nyingine.

Taka ya Chuma, shaba, risasi, karatasi, plastiki, alumini, mpira na kioo huweza kurejelezwa na kutumiwa tena kama malighafi kwa mara nyingine. Taka ya elektroniki na mafuta pia huweza kurejelezwa kwa urahisi. Kurejelezwa kwa taka hii husaidia katika kulinda rasilimali.

Kando na kulinda maliasili kurejeleza kwa taka pia huchangia katika kupunguza kiwango cha nishati kinachotumiwa katika mchakato wa kutengeza bidhaa viwandani. Faida nyingine ya kurejeleza ni kupunguza kiasi cha taka ngumu ambayo hukusanywa. Kwa njia hii, kupunguza uharibifu wa mazingira kupitia taka ngumu na pia kupunguza kiasi cha eneo la akiba linalohitajika katika nafasi ya kuhifadhi taka.

Hatua ya kwanza katika utaratibu wa kurejeleza ni kutenganishwa kwa taka inayoweza kurejelezwa na kuwekwa katika sehemu tofauti na taka ambayo haiwezi kurejelezwa. Hatua hii ni muhimu sana katika mchakato wa kurejeleza na ni jambo muhimu sana kwa taka inayoweza kurejelezwa kuwekwa katika pipa maalum.

Kwa mbinu ya kurejeleza tunaweza kuhifadhi mali asili na kutumia nishati kwa njia mwafaka zaidi.


Tagi:

Habari Zinazohusiana