Tebboune asisitiza kuzingatia demokrasia serikalini

Rais wa Algeria asema kuwa atachukua maamuzi kulingana na demokrasia baada ya matokeo ya uchaguzi

1656718
Tebboune asisitiza kuzingatia demokrasia serikalini

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune alisema kuwa kwa kuzingatia matokeo yoyote ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini, atachukua maamuzi kulingana na demokrasia.

Tebboune alifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika mji mkuu wa Algiers na kusema kwamba alikuwa na matumaini juu ya waliojitokeza katika uchaguzi wa bunge.

Akibainisha kuwa wale waliosusia uchaguzi wako huru kwa mitazamo yao, Tebboune alisema kwamba ataheshimu matokeo ya uchaguzi wakati akiunda serikali.

Tebboune pia alisema,

"Vyovyote itakavyokuwa kwenye matokeo ya uchaguzi, tutafanya maamuzi ambayo yanaambatana na demokrasia."

Zaidi ya wapiga kura milioni 24 waliojiandikisha nchini Algeria walikwenda kupiga kura ili kuwachaguwa wagombea 407 watakaowawakilisha katika Bunge la Umma la Kitaifa.

Wagombea zaidi ya 22,000 wanaojumuisha 10,468 kutoka vyama 28 vya siasa na 12,086 kutoka kwa vyama huru, wanagombea viti 407 katika bunge la kitaifa.Habari Zinazohusiana