Operesheni dhidi ya Al-Shabaab Somalia

Magaidi 10 wa kundi la Al-Shabaab waangamizwa kwenye operesheni iliyoendeshwa nchini Somalia

1656700
Operesheni dhidi ya Al-Shabaab Somalia

Magaidi 10 wameripotiwa kuuawa katika operesheni iliyoendeshwa dhidi ya shirika la kigaidi la Al-Shabaab nchini Somalia.

Katika taarifa ya redio ya jeshi la Somalia, iliripotiwa kuwa operesheni iliendeshwa dhidi ya shirika hilo katika mkoa wa Hiiraan, katikati mwa nchi.

Taarifa zaidi lieleza kuwa magaidi 10 wa shirika hilo waliangamizwa wakati wa operesheni hiyo, na magaidi wengine wengi wa Al-Shabaab walitoroka na majeraha.

Ilibainika kuwa hakuna mwanajeshi yeyote aliyejeruhiwa katika operesheni ya Hiiraan, ambayo ni mwendelezo wa operesheni dhidi ya Al-Shabaab iliyoanzishwa katika mkoa wa Hirshabelle.Habari Zinazohusiana