Kwa mara ya kwanza Kenya yafanya sensa ya wanyama

Lengo ni kuzuia ujangili

1636078
Kwa mara ya kwanza Kenya yafanya sensa ya wanyama

Kenya, kwa mara ya kwanza katika historia yake, imeanza kuhesabu idadi ya kitaifa ya wanyama pori porini.

Huduma ya Wanyamapori ya Kenya (KWS) imesema kuwa sensa hiyo, ambayo ilianzia katika Hifadhi ya Kitaifa ya Shimba Hills, inakusudia kujua idadi na usambazaji wa wanyamapori nchini.

KWS ilibaini kuwa helikopta pia zitatumika katika sensa.

Waziri wa Utalii wa Kenya Najib Balala amesema kuwa lengo la utafiti huo ni kugundua spishi zilizo hatarini na kuzuia ujangili.

Mamia ya spishi za wanyama pori wanaishi katika makazi yao ya asili kwenye mbuga nyingi za kitaifa na hifadhi nchini Kenya.Habari Zinazohusiana