Mapigano yalipuka upya mjini Tripoli

Mapigano baina ya vikosi vya serikali halali inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa na majeshi ya Hafter yalipuka upya baada ya kusimama kwa siku mbili

Mapigano yalipuka upya mjini Tripoli

Mapigano baina ya serikali inayotambuliwa na jamii ya kimataifa na majeshi ya Halifa Hafter yaliyokuwa yamesimama kwa siku mbili, yameibuka upya mashariki mwa mji waTripoli  nchini Libya.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya nchi hio mapigano makali baina ya pande hizo zinazohasimiana yametokea katika eneo la El Aziziye ambako unapatikana uwanja wa ndege wa zamani wa kimataifa wa Tripoli.

Jumatano iliyopita shirika la afya duniani liliripoti kwamba mapigano yaliyodumu kwa muda wa mwezi mmoja mjini Tripoli na maeneo ya karibu yamesababisha vifo vya watu 443.Habari Zinazohusiana