Boko Haramu wazidi kuiandama Nigeria

Askari watano wameuawa katika mashambulizi ya silaha yaliyofanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Boko Haramu wazidi kuiandama Nigeria

Askari watano wameuawa katika mashambulizi ya silaha yaliyofanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Msemaji wa jeshi Naibu Kanali Ezindu Idima amesema kuwa watu watano wamepoteza maisha katika shambulizi hilo lililotokea katika kijiji cha Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Idima amesema kuwa idadi kubwa ya magaidi wameuawa katika mapigano yaliyotokea baada ya shambulizi hilo.

Watu zaidi ya 20,000 wameuawa katika vurugu ambazo zimekuwa zikifanyika na Boko Haram nchini Nigeria tangu miaka ya 2000.

Tangu 2015, kundi hilo limefanya mashambulizi katika nchi jirani kama vile Cameroon, Chad na Niger.

Watu angalau 2,000 walipoteza maisha yao katika mashambulizi ya kundi hilo katika Bonde la Ziwa la Chad.Habari Zinazohusiana