Sisi na uwezekano wa kuendelea kubaki madarakani hadi 2030

Bunge la Misri limepitisha pendekezo la mabadiliko ya katiba lililtolewa na Rais Sisi na hivyo kumpa uwezekano wa kuwa madarakani hadi mwaka 2030

Sisi na uwezekano wa kuendelea kubaki madarakani hadi 2030

Nchini Misri, Rais  wa  nchi hio Abdulfettah es-Sisi apendekeza kwa bunge yafanyike mabadiliko ya katiba ili aweze kuendelea kubaki madarakani mpaka mwaka 2030.

Kwa mujibu wa gazeti la nchi hio El-Ahram, katika kura 596 zilizopigwa na bunge la nchi hio kuhusiana na pendekezo hilo. Wabunge 22 walipinga, 1 hakupiga kura, 531 walikubali pendekezo hilo.

Kwa minajili ya kura hizo mabadiliko yamefanyika kwenye katiba  ya nchi na kipengele tajwa kimekuwa kama ifuatavyo; “ Kutokana na kwamba Rais aliyepo madarakani alianza kutumikia kipindi chake baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mwaka 2018, miaka 6 ikipita atamaliza muda wake na baada ya hapo anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka 6”.  Habari Zinazohusiana