Silaha wakati wa vita vya Istanbul

Je, unajua kwamba mizinga ya silaha mikubwa zaidi duniani ilitumiwa na utawala wa Ottoman

1422100
Silaha wakati wa vita vya Istanbul

Je, unajua kwamba mizinga mikubwa zaidi duniani ilitumiwa na utawala wa Ottoman katika vita vya Istanbul?

Ingawa baruti na mizinga vilitumika katika vita mpaka miaka ya 1453,hakuna aliyekuwa na mizinga mikubwa kama Otoman.

Wakati Istanbul ilipozingirwa na jeshi la Ottoman,Byzantine nao walikuwa wanatumia mfumo wao wa kufyatua mizingo kwa kutumia poda nyeusi,lakini silaha hizi zilisababisha uharibifu mkubwa kwenye kuta zao.

Mizinga hiyo ya jeshi ilikuwa na mita 8.75 na ilikuwa na uwezo wa kubeba kilo 544 za risasi.

Ilichukua masaa matatu kujaza na iliweza kurusha risasi mara tano hadi sita kwa siku.

Vifaa hivi vilitumika hata baada ya vita,miaka 354 baada ya ushindi wa Istanbul.

Meli za Uingereza zilipojaribu kuvuka Dardanelles zilishambuliwa vibaya na kulazimika kuondoka kutokana na athari kubwa iliyotokea.

Mfano wa mizinga hii ilizawadiwa kwaUingereza na Sultan Abdulaziz miaka ya 1870.Habari Zinazohusiana