Leo katika historia

Victor Hugo apoteza maisha, tetemeko kubwa zaidi China na Chile, Richard Nixon atembelea USSR

1422105
Leo katika historia

22 / Mei / 1885 Mwandishi wa Ufaransa, Victor Hugo, ambaye alipata umaarufu ulimwenguni na riwaya yake "Masikini",alipoteza maisha huko Paris akiwa na umri wa miaka 83.

22 / Mei / 1927 Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.9 lilitokea katika mkoa wa Xining wa China.Watu takriban elfu 41 walipoteza maisha.


22 / Mei / 1960 Tetemeko la ardhi linalojulikana katika historia kama tetemeko kubwa zaidi lilitokea Chile. Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.5 lilichukua kama dakika 3. Tetemeko hilo lilifikia urefu wa mita 25 katika bahari na kusababisha Tsunami katika pwani ya Afrika Mashariki na kisiwa cha Hawaii.Takriban watu 5000 walipoteza maisha.


22 / Mei / 1972 Kwa mara ya kwanza, Rais wa Marekani alifanya ziara rasmi katika Umoja wa Kisovyeti.Rais wa Marekani Richard Nixon aliyetaka kupunguzwa kwa silaha za nyuklia alitembelea Moscow baada ya kualikwa na kiongozi wa USSR Brezhnev,kusaini mkataba wa kwanza wa SALT.Habari Zinazohusiana