Mbuzi wa Ankara na Sufi

Mbuzi wa Ankara asili yao ni Asia ya kati, waliletwa Anatolia na katika karne ya 13 na  na wahamaji wa kituruki waliohamia eneo hilo

1383560
Mbuzi wa Ankara na Sufi
ak2.jpg

Mbuzi wa Ankara asili yao ni Asia ya kati, waliletwa Anatolia na katika karne ya 13 na  na wahamaji wa kituruki waliohamia eneo hilo. Sifa walizonazo mbuzi hao hivi sasa wamezipata wakiwa Anatolia ya kati. Mbuzi wa Ankara ni wanyama wazurı na wakubwa kıası ambao hukua katıka mazıngıra ya mvua chache na halı ya hewa ya ukavu.

Katıka karne ya 20, mbuzi wa Ankara walikuwa wakifugwa Ankara na maeneo jirani pekee, katika tarehe tofauti mbuzi wa Ankara wakapeleka katika mataifa tofauti lakini katika kila taifa walikopelekwa mbuzi hawa walibaki na jina lao la asili. Sufi inayotokana na mbuzi wa Ankara ni maarufu katika matumizi ya kutengeneza mavazi. Sufi hiyo ni nyeupe, imara, inanga’aa, inanyumbulika kirahisi, imara dhidi ya joto, ni rahisi kuipaka rangi na ina sifa ya kuhifadhi joto, ni sufi ambayo haichafuki kirahisi kutokana na kuwa imenyooka na pia inateleza. Kutokana na kwamba ni rahisi kuchanganywa na pamba, manyoya ya kondoo na nyuzi za kutengeneza, sufi ya mbuzi wa Ankara ni moja kati ya mali ghafi inayotumika sana katika viwanda vya nguo.

Leo hii mbuzi wa Ankara hufugwa pia katika maeneo nje ya Uturuki ikiwemo Marekani, Lesotho, Argentina, Australia, Afrika kusini na Newa Zealand.Habari Zinazohusiana