Je wajua kama muziki ni tiba ?

Tiba kwa kutumia muziki ina historia ndefu kama vile utabibu wenyewe, Je wajua kwamba katika ustaarabu wa Asia ya kati na Anatolia tiba za aina hii zilitumika ?

Je wajua kama muziki ni tiba ?

Katika tamaduni za kale za kirumi, muziki ulionekana kuwa ni chanzo cha kila wema na ulitumika katika kutakasa  na kuelimisha roho. Kwa upande wa waturuki alikuwepo mganga mmoja wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la Baksi na alikuwa akitoa tiba kwa kutumia muziki.

Katika dunia ya waturuki na waislamu tiba kwa kutumia muziki ba hasa  mahospitalini zilianza kutumika katika karne ya 9, Kadiri muda ulivyopita tiba hizo zilizidi kuendelezwa.

Katika zama za kati wakati magonjwa ya akili yalikuwa hayahesabiki kama magonjwa katika mataifa ya magharibi huku waliokuwa na magonjwa hayo wakipewa mateso. Waturuki wao waliyakubali magonjwa ya akili kama miongoni mwa wagonjwa na walitoa umuhimu mkubwa katika afya ya akili, walitoa umuhimu mkubwa katika tiba ya magonjwa ya akili. Ibn Sina alitumia tiba ya muziki kutibu magonjwa ya akili. Tiba hiyo aliyotumia Ibn Sina iliendelea kutumika katika kipindi cha dola la Ottomania.

Siku hizi pia, muziki ni moja ya njia za tiba zinazotumika. Ni moja ya tiba saidizi zinazotumika katika tiba ya maradhi mbalimbali kama vile sonona, msongo wa mawazo, hasira, mshtuko, kukosa usingizi, kupoteza usikivu, maumivu ya kichwa, shingo, kiuno na viungo, kisukari, machachari,kichwa ngumu na matatizo ya kujifunza.


Tagi: waturuki , tiba , Muziki

Habari Zinazohusiana