Leo katika Historia

wachezaji 7 wa timu ya soka ya Manchester united wapoteza maisha

Leo katika Historia

Februari.6.1952             Malkia Elizabeth wa 2 ashika hatamu mara baada ya kifo cha baba yake mfalme George wa 6 . Septemba .9. 2015 Malkia Elizabeth 2 alivunja rekodi ya dunia ya kutawala muda mrefu zaidi baada ya utawala wake kuuzidi muda ule wa Malkia Victoria.

          ****

Februari.6.1958              Ajali ya ndege yatokea katika uwanja wa ndege wa Munich, watu 23 wakiwemo wachezaji 7 wa timu ya soka ya Manchester united wapoteza maisha.                                               

****

Februari.6.1983               Klaus Barbie,  kamanda wa vikosi vya Ujerumani ya kinazi “Gestapo” aliyejulikana kama “mchinjaji wa Lyon” kutokana na ukatili wake wakati wa vita vya 2 vya dunia. Atokea mbele ya hakimu nchini Ufaransa na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani, kwa  makosa aliyofanya dhidi ya ubinamu.

*****

Februari.6.2004               Mlipuko watokea katika kituo cha treni cha Moscow. Katika Tukio hilo ambalo baadae lilifahamika kuwa ni la kigaidi, watu 40 walipoteza maisha huku 129 wakijeruhiwa.

 

 

 Habari Zinazohusiana