Je wajua kwamba chai ya asili “Adaçayı”, inayoota nchini Uturuki ina faida nyingi kwa afya ?

Huimarisha mfumo wa kinga za mwili na hivyo kutoa kinga imara dhidi ya magonjwa ya kudumu

Je wajua kwamba chai ya asili “Adaçayı”,  inayoota nchini Uturuki ina faida nyingi kwa afya ?

Chai ya kisiwani “Adaçayı”, ni jina la ujumla ya mimea aina ya Salvia inayomea katika nchi za Mediterenea. Katika kundi la mimea hii aina 900 tofauti. Miongoni mwa aina 97 zinazooteshwa nchini Uturuki aina 51 asili yake ni Uturuki.

Adaçayı  ni mmea wa miujiza wenye faida zisizohesabika katika afya ya binadamu.  Madaktari wa jamii wamekuwa wakiutumia mmea huu kwa kipindi kirefu kutibu homa ya mafua na mchafuko wa tumbo. Miongoni mwa kemikali zinazopatika katika mmea huu ni antioksidant zinazosaidia kuimarisha mfumo wa kinga za mwili na hivyo kutoa kinga imara dhidi ya magonjwa ya kudumu. Utafiti unaonyesha kwamba mmea huu hupunguza kiwango cha kolesterol mbaya mwilini na kuongeza kiwango cha kolesterol nzuri mwilini. Chai hii pia ina faida kwa afya ya ubongo pamoja na kuimarisha kumbukumbu.

Pamoja na “adaçayı” na bidhaa nyingine zinazo tokana na mmea huu kuwa na faida nyingi kwa afya, pia kuna madhara kiasi yanayoweza kusababishwa  na matumizi ya mmea huu. Inashauriwa kwa mama wajawazito na wanaonyesha kutotumia kwa wingi chai hii. Kwa wale wanaotumia dawa za kisukari na zile za kushusha kolestorol wanashauriwa kuwa makini wakati wa kutumia bizaa zinazotokana na chai hii. Adaçayı,  hutumiwa zaidi nchini Uturuki kama chai ya mimea. Majani ya kijani kibichi hutumiwa kama mbogamboga pamoja na kuleta harufu na ladha nzuri  katika vyakulavya nyama na samaki. Mafuta ya asili yanayopatikana katika majani ya mmea huu hutumika viwandani kutengeneza dawa na vipodozi.Habari Zinazohusiana