Je wajua kama kufuga paka kuna faida nyingi katika afya ya binadamu ?

Watafiti wa mahusiano baina ya binadamu na wanyama wamebaini kwamba paka huleta faida katika afya ya binadamu

Je wajua kama kufuga paka kuna faida nyingi katika afya ya binadamu ?

Wanasayansi wanaotafiti uhusianao wa binadamu na wanyama, wamebaini kwamba kufuga paka kuna faida katika afya ya binadamu. Nyumba ambayo kuna paka mawasiliano ya kijamii huongezeka, kucheka, kucheza na kufanya mazoezi huongezeka hivyo basi husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Pia huimarisha mfumo wa kinga mwilini.

Ishara ya kale zaidi  inayofahamika ambayo inathibitisha uhusiano baina ya binadamu na paka ni ile ya Kupro ambako katika kaburi la binadamu ilipatikana mifupa ya paka iliyokuwa na umri wa miaka 9.500...Wakulima wa kwanza kutokea Anatolia kwa kutumia boti walipeleka paka wa porini mpaka kisiwani. Kupro hakukuwa na paka hapo mwanzo. Hali hii inaonyeshwa kwamba uhusiano baina ya binadamu na paka katika eneo la Anatolia una zaidi ya miaka 10,000. Hiyo inaonyesha kwamba binadamu na paka waliishi pamoja tangu kilimo kilipoanza.

Miongoni mwa paka watanashati zaidi ni paka wa Van. Paka hawa wa aina yake wanaishi kuzunguka ziwa Van. Macho ya paka hawa yana rangi tofauti ikiwa jicho moja ni la rangi ya samawati na jingine ni la rangi ya kahawia. Paka hawa wana mkia mnene na manyoya mengi rangi nyeupe.Wanapeda sana maji na kuogelea. Paka wa Van walisajiliwa rasmi kama ni mali ya Van mnamo April 22, 2006.Habari Zinazohusiana