Kipindi kipya cha ushirikiano kati ya Uturuki na Urusi

Uchambuzi kutoka katika shirika la utafiti wa kisiasa, uchumi na jamii SETA na  Mchambuzi CanACUN

Kipindi kipya cha ushirikiano kati ya Uturuki na Urusi

Ushirikiano katika ya Uturuki na Urusi ameanza upya katika kipindi kigumu mwaka 2015.

Mataifa hayo yalikuwa katika mvutano.  Hali hiyo ya vuta nikuvute kati ya Uturuki na Urusi  ilibadilika  katika muda mfupi na kuonekana ushirikiano kupiga   hatua katia  ushirikiano wa kisiasa, diplomasia, ulinzi na uchumi

Ushirikiano katika viongozi wa mataifa hayo mawili  ulifufuka  kwa haraka  licha ya kuwa ulikuwa katika hali isioridhisha. Baada ya kuona kuwa kuna maslahi kati ya mataifa hayo mawili , mataifa hayo hayakuwa na budi kushirikiano. 

Licha ya kuwa mataifa hayo  yanashirikiana katika nyanja tofauti vile vile  kuna tofauti ambazo zinashuhudiwa katika  masuala mengine tofauti.

Uchambuzi kutoka katika shirika la utafiti wa kisiasa, uchumi na jamii SETA na  Mchambuzi CanACUN.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa Uturuki na Urusi ni mataifa mbayo yamepigwa atua katika ushirikiano. Putin amesema kuwa  ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili  unaleta manufaa mapya kati ya mataifa hayo . kuimarika kwa ushirikiano bain aya mataifa hayo mawili  ni mabadiliko makubwa katika diplomasia.

 Ushirikiano katika nyanja tofauti kati ya Uturuki na Urusi unashuhudiwa katika sekta ya nishati na ucchumi , sekta ambazo  zina umuhimu mkubwa katika ushirikiano.

Waziri wa zamani wa  fedha wa Urusi  Zadornov  amesema kuwa kuna ushirikiano  mzuri  kati ya Uturuki na Urusi katika sekta ya uchumi. Uturuki  ni  mshirika  wa Urusi  miongoni mwa mataifa 10 ambayo yanashirikiano katika sekta ya biashara.

Kutoka na kuwa miongoni mwa mataifa mbayo yanashirikiana na Urusi katika biashara  ,  kitengo cha kodi na ushuru cha Urusi kimesema kuwa  katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya mwaka 2018 katika biashara Uturuki imeongeza  zaidi ya asilimia 37 ya biddhaa zake Urusi.  Kiwango cha dola   zaidi ya  bilioni 13,3. Uturuki imekuwa mshirika muhimu wa Urusi katika sekta ya biashara.

Watalii  kutoka nchini Urusi wanaotembelea nchini  Uturuki katika kipindi cha kiangazi wana umuhimu  mkubwa katika  ushirikiano kati ya Uturuki na Urusi. Utıuruki ina nufaika katika sekta yake ya uchumi kutokana na ujio wa watalii wengi kutoka Urusi.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu  amefahamisha kuridhishwa na idaidi hiyo ya watali na kuendelea kusema kuwa ana imani kuwa idadi hiyo itaendelea kuongezeka.

Miradi tofauti kama mradi wa  kituo cha nishati cha Akkuyu mi moja miongoni mwa miradi ya ushirikiano kati ya Uturuki na Urusi katika sekta ya nishati.

Mradi wa kituo cha nyuklia cha Akkuyu kitakuwa na jawabu la  mahitaji ya nishati  kati ya Uturuki na maaifa washirika  wake.   Sekta ya nishati kwa uTuruki ni moja miongoıni mwa sekta ambazo zinategemewa katika kuimarisha uchumi wa Uturuki. 

Sekta hiyo inainua uchumi  kwa asilimia 10. Vile vile mradi wa Stream una mchango mkubwa katika uchumi wa Uturuki. Mradi huo aidha miradi hiyo itakuwa oia na mchango katika mataifa ya Balkans katika awamu yake ya pili. Itakuwa ni   atua muhimu katika  mpango wa kimkakati katika usafirishaji wa nishati na gesi kutoka Uturuki.

 ushirikiano katika sekta ya uchumi kati ya Uturuki na Urusi  unazidi kuimarika ikiwemo pia ushirikiano katika sekta ya nishati na gesi asilia. Uturuki imenunua mfumo wa kujşhami na makombora kutoka Urusi ikiwa moja ya hatua ya Uturuki kulinda anga lake na mashambulizi yeyote  yatakayo kuwa yakilenga  usalama wa Uturuki.

Mfumo wa kujilinda na makombora wa S-400 ni ishara pia kuwa mataifa hayo yanashirikiana katika sekta ya ulinzi.

Mfumo huo wa  S-400 Uturuki itakabidhiwa na Urusi ifikapo mwaka 2019.

Shirika ambalo linahusika na utengezaji wa silaha nchini Urusi Rosten na mkurugenzi wake Viktor Kladov   amesema kuwa mfumo huo  malengo yake ni kuimarisha ushirikiano   katika sekta ya ulinzi kati ya Uturuki na Urusi.

Mataifa hayo tayari yamepiga hatua katika suaşla hilo.

Mkurugenz huyo ameendelea kusema kuwa haoni  tofauti yeyote  au kizuizi  kwa kushirikiana katika sekta ya ulinzi na  Uturuki.

Ushirikiano kati ya Uturuki na Marekani umeonekana kuyumba baada ya Uturuki kuchukuwa uamuzi wa kununua  mfumo wa kujihami na makombora wa S-400. Uturuki ni mshirika katika mradi wa  ndege za kivita aina ya F-35.

Waziri wa amambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu alifahamisha kuwa  Uturuki haikuwa na budi kununua mfumo huo  kwa ajili ya ulinzi. 

Uturuki ilikuwa na lengo la kutaka kununua mfumo huo  kutoka katika taifa mshirika  katika shirikisho la kujihami la Magharibi NATO.

Suala zima kuhusu kundi la wahaini wa FETÖ,  mapambano ya Uturuki dhidi ya kundi la PKK na tawi lake la YPG na sasa mchungaji Brunson ushirikiano kati ya Uturuki na Marekani umeonekana  kuingia katika hali ambayo sio mataifa washirika na wanachamwa NATO.

Rais wa Marekani  Donald Trump amechukuwa uamuzi wa kuiwekea  Uturuki  vikwazo  na uamuzi huo umepelekea  ushirikiano kati ya Uturuki na Marekani   kuyumba.  Waziri wa ammbo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu  amekuwa akizungumzia kuhusu ushirikiano kati ya Marekani na Uturuki na ushirikiano uliopo pia kati ya Uturuki na Urusi.

Ushirikiano kati ya Uturuki na Urusi ni ushirikiano ambao unaonekana kutowafurahisha baadhi ya watu. Kwa kweli hali ya ushirikiano kati ya Uturuki na Urusi    ni ushirikiano unaoshangaza.

Licha ya kuwa na tofauti ushirikiano bado ni ushirikinao huku mazungumzo yakiendelea katika masuala ambayo ni yanaitaji mazungumzo na makubaliano.

Kuhusu suala zima la Syria, Uturuki na Urusi   zimeshirikiana ili kuhakikisha kuwa amnai inarejea nchini Syria.  Mataifa yaho yalipendekeza mazungumzo ya amani mjini Astana ili kutatua mzozo wa Syria.

Kuna umuhimu mkubwa  ambao hauna mjadala kwa Uturuki.  Uturuki iliomba kununua mfumo wa kujşhami kutoka  taifa mshirika wa NATO  na kuwekewa masharti ambayo hayakuwa na umuhimu kwa taifa mwanachama. Uturuki ni taifa mwanacha wa NATO ambae pia anashiriki katika  juhudi za kujihami na kulinda usalama  barani  Ulaya. 

Uturuki na Marekani yamejipata katika hali ya vuta ni kuvuti kutokana na ushirikiano uliogunduliwa kati ya Marekani na kundi la wanamgambo wa kundi la YPG ambalo bila shaka ni tawi la wanamgambo wa PKK , kundi la kigaidi ambalo linashambulia  ardhi ya Uturuki na kusababisha  maafa. S

uala  jingine ambalo liliibua utata  ni kukamatwa kwa mchungaji Brunson amabe ametuhumiwa na serikali ya Uturuki kushirikiana na  kundi la kigaidi. Kukamatwa kwake kumepelekea  mgogoro  kati ya Marekani na Uturuki.  Rais wa Marekani Donald Trump  amechukuwa uamuzi wa kuiwekea vikwazo Uturuki.  Kutokana na uamuzihuo  waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu amesema kwamba ushirikiano uliopo kati ya Uturuki na Urusi ni ushirikiano ambayo  hauridhishi baada ya watu.

Ushirikiano kati ya Uturuki na  Urusi ni ushirikiano ambao  unaendelea kuimarika licha ya kuwa na utofauti katika masuala lkadhaa.  Moja miongoni wa tofauti hizo ni mzozo wa Syria. Mazungumzo ya Astana ni kwa lengo  la kurejesha amnai ya kudumu nchini Syria.  Kusitisha mapigano İdlib na maeneo mengine  nchini humo ni matumaini ya Utıuruki katika mazungumzo. Iwapo kutaanzishwa operesheni Idlib  Uturuki inahofia wimbi la wakimbizi hivyo basi ni wajibu wa  Urusi kumzuia mshika wake  kutoanza mashambulizi  kwa kuwa maddhara yake yatakuwa ni makubwa.

Suala jingine ni kuhusu Krimea, Uturuki haiungi mkono  mwenendo wa Urusi katika jimbo la Krimea.

Uchambuzi kutoka katika shirika la utafiti wa kisiasa, uchumi na jamii SETA na  Mchambuzi CanACUNHabari Zinazohusiana