Elimu ya juu nchini Uturuki

Elimu ya juu nchini Uturuki,chuo cha Anadolu

712565
Elimu ya juu nchini Uturuki

Karibu kwa mara nyingine katika kipindi cha elimu ya juu ya Uturuki.Leo tunakuleteeni chuo maarufu duniani na Uturuki nzima.Chuo cha Anadolu kilichopo mji wa Eskişehir.Mji wa Eskişehir ni mji mzuri na ulioendelea na kwa zama za sasa za treni za umeme ni masaa machache tu kutoka mji huo kuelekea miji mikubwa kama Ankara na Istanbul.Mji huo hupendwa na wanafunzi n ani mji wa wanafunzi.Chuo cha Anadolu kilianzishwa mnamo mwaka 1982 na kimekuwa kikikua kwa kasi mpaka wa hii leo.Chuo cha Anadolu ni chenye ubora mkubwa na ni cha kisasa.Chuo hiki kipo mjini Eskişehir na kina campus mbili huku kikiwa na faculty kumi na saba.Chuo hicho kinatoa elimu ya kawaida kama chuo na elimu kupitia mtandao.Chuo hicho hujulikana kama chuo bora kwa kutoa elimu kupitia mtandao nchini Uturuki.

 

Chuo hiki kimekuwa kikitoa wanafunzi wengi bora katika masuala ya teknolojia kwa miaka mingi.Chuo hiki ni chuo chenye uwezo mkubwa wa kutoa elimu bora na ya kisasa inayokubalika.Mazingira ya chuo yanamfanya mwanafunzi asome zaidi kwani kina maktaba kubwa yenye kila aina ya vitabu na hufunguliwa masaa ishirni na manne.Baada ya saa kumi nam bili jioni,wanafunzi wanaobaki kusoma maktaba hupewa chai,kahawa na supu bure.Vilevile chuo hiki kinauwanja mkubwa wa kufanya mazoezi na michezo ya olimpiki na kwa wale wapendao kuogelea basi kuna swimmingpool kubwa na ya kutosha.Vyakula katika chuo hicho ni vya kiwango cha juu.Vyakula hutolewa wakati wa mchana na usiku.Chuo kina wanafunzi takriban zaidi ya elfu nne kutoka katika nchi mbalimbali na wanaamini chuo cha Anadolu kitawapatia elimu ya kiwango cha juu.Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya www.anadolu.edu.tr. Huduma zinatolewa kwa lugha ya kituruki na kiingereza.

Tukutane tena Juma lijalo kwa taarifa za vyuo vingine.Habari Zinazohusiana