Uturuki yajibu Ugiriki kwa Navtex

Uturuki yatangaza zoezi la Navtex katika Bahari ya Aegean baada ya Ugiriki kukiuka Mkataba wa Athens

1663461
Uturuki yajibu Ugiriki kwa Navtex

Uturuki ilijibu kwa Navtex tangazo la Ugiriki la uwanja wa mafunzo ya kijeshi katika mipaka ya kimataifa ya Bahari ya Aegean kwa zoezi la kutekelezwa msimu wa utalii, kinyume na Mkataba wa Athens ambao ulisainiwa.

Uturuki, ilitangaza maeneo ya mafunzo katika mipaka ya kimataifa ya Bahari ya Aegean kwa zoezi la (Navtex) la tarehe 22 Juni.

Kulingana na taarifa iliyopokewa kutoka kwa vyanzo vya usalama, katika Mkataba wa Makubaliano wa Athens uliosainiwa kati ya Uturuki na Ugiriki mnamo 1988, iliamuliwa kutofanya mazoezi katika mipaka ya kimataifa ya Bahari ya Aegean na kutangaza uwanja wa mazoezi ya kijeshi wakati wa shughuli nyingi za msimu wa utalii kati ya tarehe 15 Juni na 15 Septemba.

Kwa kuzingatia kipindi cha Kusitisha mazoezi kilichoanzishwa na Mkataba wa Makubaliano, Uturuki haikutoa tangazo la zoezi katika mipaka ya kimataifa ya Bahari ya Aegean kati ya tarehe 15 Juni na 15 Septemba wakati wa kupanga shughuli za mafunzo ya operesheni  ya mwaka 2021.

Ugiriki, kwa upande mwingine, haikutii makubaliano na ilitangaza eneo la mazoezi kwa mwaka huu, pamoja na kipindi kilichositishwa. Licha ya mtazamo wa heshima wa Uturuki na mipango ya kidiplomasia juu ya Kusitishwa, Ugiriki haikufanya mabadiliko yoyote katika maeneo ambayo ilitangaza kukiuka usitishaji.

Uturuki, ambayo inafuata kwa karibu mazoea ya Ugiriki yaliyokiuka usitishaji, imekuwa na jukumu la kujibu zoezi hilo katika mfumo wa kuzingatia makubaliano. Hivyo basi, matangazo yaliyochapishwa na Uturuki mnamo Juni 22, 2021, yalieleza  maeneo ya mafunzo na mazoezi katika mipaka ya kimataifa ya Bahari ya Aegean.Habari Zinazohusiana