Ziara ya wajumbe wa Uturuki nchini Libya

Fahrettin Altun afanya mkutano wa mazungumzo na wajumbe wa Libya wakati wa ziara yao rasmi

1656920
Ziara ya wajumbe wa Uturuki nchini Libya

Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano wa Ofisi ya Rais Fahrettin Altun, alisema kuwa wakati wa ziara yake nchini Libya, walifanya mkutano wa mazungumzo muhimu kwa umoja, amani na utulivu wa nchi hiyo.

Katika ujumbe wake kwenye akaunti yake ya Twitter, Altun alisema kuwa walifanya mikutano muhimu na wajumbe walioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Mevlüt Çavuşoğlu nchini Libya, ambapo walikwenda kutathmini maendeleo ya hivi karibuni, kwa umoja, amani na utulivu wa nchi hiyo.

Akibainisha kwamba walikutana na Ammar El-Lafi, Waziri wa Nchi wa Mawasiliano na Maswala ya Siasa nchini Libya, Altun alisema:

"Tulikuwa na mkutano wenye tija na kuimarisha ushirikiano wetu katika uwanja wa mawasiliano. Uturuki, chini ya uongozi wa Rais Recep Tayyip Erdoğan, itaendelea kuwepo katika kanda yake kama mhusika bora, anayeaminika na mwenye nguvu na kuchangia katika uimarishaji wa amani na utulivu wa kikanda na duniani. "Habari Zinazohusiana