Rais Erdoğan kuelekea Brussels leo hii

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan kuelekea Brussels Ubelgiji kwa ajili ya mkutano wa NATO

1656937
Rais Erdoğan kuelekea Brussels leo hii

Rais Recep Tayyip Erdoğan atakwenda Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji, kuhudhuria Mkutano wa NATO, utakaofanyika kesho.

Rais Erdoğan atafanya mikutano ya pande mbili na viongozi wa nchi wanachama wa NATO akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa Lithuania Gitanas Nauseda, Rais wa Latvia Egils Levits, Waziri Mkuu wa Ujerumani Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kiryakos Mitsotakis.

Erdoğan pia amepanga kukutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte.

Mbali na muungano katika NATO, uhusiano wa pande mbili na maswala ya kikanda yanatarajiwa kuwa kwenye ajenda wakati wa mazungumzo.

Mkutano wa Erdoğan na Biden utakuwa mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili baada ya uchaguzi wa Biden kuingia madarakani kama Rais wa Marekani.

Ajenda ya kipaumbele ya wajumbe wa Uturuki walioongozwa na Rais Erdoğan katika Mkutano wa NATO itakuwa heshima kwa haki ya uhuru wa Uturuki na umuhimu wa usalama kuhusu maendeleo kwenye kanda yake. Katika mkutano huo, uamuzi wa Uturuki juu ya maswala haya utasisitizwa.

Itatiliwa mkazo kuwa Uturuki ni nchi mwanachama inayotimiza majukumu yake katika upeo wa muungano, na maombi ya ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi na uhusika katika mizozo ya kibinadamu vitazunguzmiwa.Habari Zinazohusiana