Mkutano wa İbrahim Kalın na Jake Sullivan

Msemaji wa Rais İbrahim Kalın afanya mkutano na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan

1656720
Mkutano wa İbrahim Kalın na Jake Sullivan

Msemaji wa Rais İbrahim Kalın, alifanya mkutano wa mazungumzo kwa njia ya simu na Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan.

Wakati wa mkutano huo, maendeleo ya kikanda, hali ya Afghanistan, Syria, Libya, Mediterania ya Mashariki na Cyprus, pamoja na uhusiano kati ya nchi mbili yalitathminiwa.

Maelezo ya mkutano wa nchi mbili utakaofanyika ndani ya wigo wa Mkutano wa NATO kati ya Rais Recep Tayyip Erdoğan na Rais wa Marekani Joe Biden pia yalijadiliwa.

Ilisisitizwa kuwa uhusiano kati ya Uturuki na Marekani ambao ni washirika wawili wa NATO wenye historia ndefu, unapaswa kukuzwa na ajenda nzuri na kulenga ushirikiano wa kimkakati.

Ilikubaliwa kuwa maswala yote yanayohusu uhusiano wa Uturuki na Marekani yanapaswa kushughulikiwa kwa uelewa wa masilahi na kuheshimiana.Habari Zinazohusiana