Akar akutana na maafisa wa kijeshi wa Libya

Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa Hulusi Akar afanya mkutano na maafisa wa kijeshi wa Libya

1656951
Akar akutana na maafisa wa kijeshi wa Libya

Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa Hulusi Akar alikutana na maafisa wa kijeshi kama sehemu ya ziara yake nchini Libya.

Akar alikutana na Mkuu wa Wafanyikazi wa Usalama wa Libya, Jenerali Muhammed Ali Haddad, na Kamanda wa Jeshi la Mkoa wa Tripoli, Meja Jenerali Abdulbasit Marwan.

Baada ya mapokezi, Akar alikutana na wafanyikazi wa usalama katika Kituo cha Utawala cha Kikazi cha Libya.

Akisisitiza uhusiano wa urafiki kati ya Uturuki na Libya ambao umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi, Akar alisema kuwa Uturuki itaendelea kufanya chochote kinachohitajika  kwa umoja, uadilifu na usalama wa Libya.

Akikumbusha mashambulizi ya Haftar dhidi ya raia wasio na hatia nchini Libya, Akar pia alisema kuwa vilipuzi vilivyowekwa na kundi la Haftar mpaka kwenye vitu vya kuchezea vilisababisha vifo vya raia wengi ikiwa ni pamoja na watoto.

Akar aliongezea kusema:

"Tuna ndugu wengi wa Libya ambao walipoteza viungo vyao na wakawa mashujaa kwa sababu ya milipuko wa vilipuzi. Baadhi yao wako chini ya matibabu hapa Uturuki. Tunasimama pamoja kwa maumivu haya na dhiki za ndugu zetu wa Libya na tunajitahidi kupunguza hali hii."

Akar alimaliza kwa kusema, "Kama ndugu, kama nguvu moja na kama mwili mmoja, tuko pamoja na Libya katika kupigania haki yao."Habari Zinazohusiana