Erdoğan amkosoa Biden kwa kuuzia silaha Israel

Rais Erdoğan amkosoa Rais wa Marekani Joe Biden kwa kuidhinisha uuzaji wa silaha kwa Israel

1641052
Erdoğan amkosoa Biden kwa kuuzia silaha Israel

Rais Recep Tayyip Erdoğan amemkosoa Rais wa Marekani (USA) Joe Biden kwa kuidhinisha uuzaji wa silaha kwa Israel na kujibu hatua hiyo kwa maneno haya:  "Nyinyi mnaandika historia kwa mikono yenu ya damu."

Erdoğan alitoa taarifa baada ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri ambapo alisema,

"Mnaandika historia kwa mikono yenu ya damu. Nakumbusha tena leo kwamba tunaendelea kushika doria Jerusalem kama milioni 84. Ardhi za Palestina zinaoshwa na damu, unaiunga mkono."

"Ukweli kwamba Marekani na nchi zilizofwata zilitangaza Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel mwishoni mwa mwaka 2017 iliongeza hamu ya serikali hii ya mauaji kumwaga damu."  Erdoğan alisema.

"(Israeli) ni makatili wa kutosha kuua watoto wa miaka 5-6, kuua wanawake kwa kuwatambaza chini, kuua watu wazee. Hawalinganishwi na yeyote.’’

Ilitangazwa kwamba Biden aliidhinisha uuzaji wa silaha zenye thamani ya dola milioni 735 kwa Israel.

Rais Erdoğan pia alisema kwamba alikuwa anaona serikali ya Austria ambayo ilipandisha bendera ya Israel kwa jengo la Wizara Kuu.

"Taifa la Austria labda linajaribu kuwafanya Waislamu walipe fidia kwa Wayahudi waliowafanyia mauaji ya kimbari." Erdoğan alizungumza maneno hayo.

"Usimamizi wa Jerusalem na tume yenye wawakilishi wa dini 3 itakuwa njia sahihi zaidi na thabiti katika hali za sasa." Pia alitoa maoni.Habari Zinazohusiana