Taarifa ya Varank kuhusu chanjo ya ndani

Waziri wa Viwanda na Teknolojia Mustafa Varank atoa taarifa juu ya chanjo ya ndani ya adenovirus dhidi ya Covid-19

1639563
Taarifa ya Varank kuhusu chanjo ya ndani

Waziri wa Viwanda na Teknolojia Mustafa Varank alitoa taarifa juu ya chanjo ya ndani ya adenovirus inayotengenezwa dhidi ya virusi vya corona (Covid-19).

Alisema, "Haina madhara au haitawadhuru watu,  na ina faida zaidi na yenye ufanisi zaidi."

Varank alisema kwenye taarifa yake aliyoitoa katika mji mkuu Ankara,

"Tutakuwa katika hatua ya majaribio kwa wanadamu katika aina 2 za chanjo, 1 VLP na 1 adenovirus nchini Uturuki. Ikiwa tunaweza kupata watu wanaojitolea kwa hiari wa kutosha katika majaribio ya chanjo na ikiwa matokeo ya chanjo yatafanikiwa , tunaamini kuwa tunaweza kupata chanjo ya Uturuki ya ndani na kitaifa kabla ya mwisho wa mwaka."Habari Zinazohusiana