Soylu ampokea Johansson

Uturuki na EU

1636122
Soylu ampokea Johansson

Waziri wa Mambo ya Ndani Süleyman Soylu amempokea Ylva Johansson, Kamishna wa EU wa Maswala ya Ndani wa Tume ya Jumuiya ya Ulaya (EU), ambaye alifanya ziara ya kikazi nchini Uturuki.

Baada ya mkutano huo katika Kituo cha Uratibu wa Hali ya Usalama na Dharura (GAMER) katika mji mkuu Ankara, Johansson alisaini "Kitabu cha Heshima" na baada ya hapo mkutano na wajumbe ulianza.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuzingatia nyanja zote za ushirikiano katika uwanja wa uhamiaji na uhuru wa visa kati ya Uturuki na EU.


Tagi: #EU , #Uturuki

Habari Zinazohusiana