Virusi vya corona Uturuki

Idadi ya vifo katika mapambano dhidi ya virusi vya corona

1635324
Virusi vya corona Uturuki

Idadi ya vifo katika mapambano dhidi ya virusi vya corona (Covid-19) ndani ya masaa 24 yaliyopita imeripotiwa kuwa 365 nchini Uturuki.

Idadi ya watu wote waliopoteza maisha tangu mwanzo wa janga hilo imeongezeka hadi 41,883.

Wagonjwa 2,414 wapya waligunduliwa kati ya watu 229,491 waliofanyiwa vipimo ndani ya siku moja. Idadi ya kesi za maambukizi kwa siku ni 26,476.

Watu 35,464 walikamilisha matibabu yao na kupelekea idadi ya waliopona kuongezeka hadi 4,589,501.

Wakati huo huo, Waziri wa Afya wa Uturuki Fahrettin Koca amesema kuwa anatumai kuwa hatua mpya zilizochukuliwa zitasaidia kupunguza idadi ya vifo na wagonjwa wa Covid*19.

Uturuki ilitoa amri ya kutotoka nje kuanzia Juma lililopita mpaka hapo tarehe 17 mwezi Mei.Habari Zinazohusiana