Çavuşoğlu azungumza na Maas

Uturuki na Ujerumani

1635369
Çavuşoğlu azungumza na Maas

Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu amesema kuwa Uturuki imechukua kila tahadhari kwa ajili ya likizo salama.

Çavuşoğlu alifanya mkutano wa ana kwa ana kati ya ujumbe na Waziri wa Mambo ya nje Heiko Maas katika mji mkuu wa Berlin.

Kwenye mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari uliofanyika baada ya mkutano huo, Çavuşoğlu alisema kuwa walijadili mambo mengi ya uhusiano wa nchi mbili, maswala ya kikanda, maendeleo katika Mashariki ya Mediterania, Libya na Syria.

Akibainisha kuwa kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili kimeongeharaka licha ya janga la corona, Çavuşoğlu aliongeza kwa kusema,

"Kiwango hiki kinaweza kuongezeka hadi zaidi ya dola bilioni 40 mwaka huu.".

Akielezea kuwa makubaliano ya pamoja na Ujerumani mwaka jana juu ya utalii yalileta matokeo mazuri kwa pande zote mbili, Mevlüt Çavuşoğlu amesema kuwa Uturuki imechukua hatua zingine za kuingia salama msimu wa utalii (licha ya janga hilo), na kwamba faida za hili zimeanza kuonekana .

Katika hotuba yake, Heiko Maas amesema kuwa Ujerumani, kila wakati wanatetea uhusiano mzuri na Uturuki,

"Uturuki ni mshirika muhimu sana katika NATO. Ujerumani imekuwa ikisisitiza jambo hili kila wakati. Itakuwa na umuhimu mkubwa siku za usoni."

Waziri wa Mambo ya nje Çavuşoğlu pia alikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Horst Seehofer kupitia mkutano wa video.Habari Zinazohusiana