Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Mukhtasari wa Magazeti ya Uturuki 26.04.2021

1628213
Leo Katika Magazeti ya Uturuki

Vatan "Ujumbe wa Çanakkale kutoka kwa Rais Erdoğan"

Rais Recep Tayyip Erdoğan, katika ujumbe aliotoa wakati wa maadhimisho ya miaka 106 ya Vita vya Ardhi vya Çanakkale, alisema, "Tutaendelea kuweka roho ya Çanakkale hai na kuibeba nchi yetu kwa siku zijazo kwa nguvu zaidi."

 

Yeni Şafak "Malengo ya ugaidi yameharibiwa"

Operesheni za Pençe-Simşek na Pençe-Yıldırım dhidi ya shirika la kigaidi la PKK zinaendelea kaskazini mwa Iraq. Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa, ilielezwa kuwa "Ngome za magaidi ziliingiliwa wakati wa utekelezaji wa operesheni za Pençe-Şimşek na Pençe-Yıldırım na kikosi chetu cha Anga kiliharibu malengo ya kigaidi."

 

Star ‘‘Tatar: Uturuki ndiyo yenye sauti, hatuwezi kuruhusu haki zetu zikiukwe’’

Rais wa Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini (KKTC) Ersin Tatar, alizungumza kwenye mahojiano yaliyochapishwa nchini Ugiriki na gazeti la "Kathimerini" ambapo alielezea kuwa masilahi yao ya pamoja na Uturuki kwa kusema, "Uturuki ni nchi kubwa, yenye dhamana, na taifa mama. Ndio nchi yenye sauti."

 

Hürriyet "Mafanikio makubwa kutoka kwa Aksungur"

Rais wa Sekta ya Ulinzi İsmail Demir alitangaza kwamba Aksungur SİHA (Chombo cha Kijeshi cha Anga kisichokuwa na rubani) ilifanikiwa kufikia lengo lake katika umbali wa kilomita 30 kwa kilo 340 KGK-SİHA-82, ambayo iliifyatua shabaha kwa mara ya kwanza.

 

Sabah "Mwanaspoti wa miereka wa kitaifa Rıza Kayaalp bingwa wa Ulaya kwa mara ya 10’’

Rıza Kayaalp, mwanaspoti wa mierekawa kitaifa aliye na kilo 130 za Greco-Roman, alishinda medali ya dhahabu kwa kumshinda mpinzani wake wa Georgia Iakobi Kajaia na kuwa Bingwa wa Ulaya kwa mara ya 10 katika taaluma yake.Habari Zinazohusiana