Virusi vya Corona Uturuki

Watu 362 wapoteza maisha kwa virusi vya corona (Covid-19) ndani ya masaa 24 Uturuki

1626215
Virusi vya Corona Uturuki

Idadi ya vifo katika mapambano dhidi ya virusi vya corona (Covid-19) ndani ya masaa 24 yaliyopita imeripotiwa kuwa 362 nchini Uturuki.

Idadi ya watu wote waliopoteza maisha tangu mwanzo wa janga hilo imeongezeka hadi 36,975.

Wagonjwa 2,932 wapya waligunduliwa kati ya watu 318,839 waliofanyiwa vipimo ndani ya siku moja. Idadi ya kesi za maambukizi kwa siku ni 61,967.

Watu 52,213 walikamilisha matibabu yao na kupelekea idadi ya waliopona kuongezeka hadi 3,844,342.Habari Zinazohusiana