Familia ya Erdoğan na ya Zelenskiy zajumuika Istanbul

Rais Erdoğan na mkewe, na Rais Zelenskiy na mkewe wajumuika kwenye mlo wa pamoja mjini Istanbul

1618929
Familia ya Erdoğan na ya Zelenskiy zajumuika Istanbul

Rais Recep Tayyip Erdoğan na mkewe Bi Emine Erdoğan, walijumuika pamoja kwa mlo wa jioni na Rais wa Ukraine Vladimir Zelenskiy na mkewe Bi Olena Zelenska, waliokuja Istanbul kuhudhuria Mkutano wa 9 wa Baraza la Mkakati kati ya Uturuki na Ukraine (YDSK).

Emine Erdoğan alichapisha ujumbe kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter na kusema,

"Tulikuwa na mazungumzo mazuri na Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky na mkewe mpendwa Olena Zelenska wakati wa mlo wa jioni katika Jumba la Huber."

Picha iliyopigwa ya Rais Erdoğan, mkewe Emine Erdoğan, Rais wa Ukraine Zelenskiy na mkewe Zelenska pia iliambatanishwa na ujumbe uliotolewa.Habari Zinazohusiana