Ushirikiano kati ya Uturuki na Kuwait

Mazungumzo ya Uturuki na Kuwait

1617329
Ushirikiano kati ya Uturuki na Kuwait

Waziri wa Mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu amesema kuwa anafurahi kuwa katika makubaliano na Kuwait juu ya maswala ya mbalimbali.

Çavuşoğlu alikuwa na mkutano wa faragha na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait na Waziri wa Mambo ya Nje wa Baraza la Mawaziri Ahmed Nasır Muhammed es-Sabah, ambaye alikuwa kaika mji mkuu Ankara.

Kamati ya Pamoja ya Ushirikiano wa Uturuki na Kuwait (IOB) ambao walishiriki katika mkutano wa mawaziri hao wawili walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Akibainisha kwamba walijadili uhusiano kati ya nchi hizo mbili na maswala ya eneo na mwenzake, Çavuşoğlu alisema,

"Nimefurahiya kuwa tunakubaliana juu ya maswala ya kikanda. Lengo la nchi zote mbili katika eneo hili ni amani, utulivu, na maendeleo ya uchumi." 

Waziri wa Kuwait naye amesema kuwa nataka kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili.

 Habari Zinazohusiana