Erdoğan achaguliwa tena kama Mwenyekiti wa AK Party

Rais Recep Tayyip Erdoğan achaguliwa tena kama Mwenyekiti wa Chama cha Haki na Maendeleo (AK Party)

1607825
Erdoğan achaguliwa tena kama Mwenyekiti wa AK Party

Rais Recep Tayyip Erdoğan, amechaguliwa tena kama Mwenyekiti wa Chama cha Haki na Maendeleo (AK Party) kwa kupata kura zote 1428 halali zilizopigwa katika Mkutano wa 7 wa Baraza Kuu la Chama.

Uchaguzi wa mwenyekiti ulimalizika katika Mkutano wa 7 wa Baraza Kuu la Chama cha AK Party uliofanyika kwenye ukumbi wa Michezo wa Ankara.

Kulingana na matokeo ya uchaguzi, kura 1431 zilipigwa ambapo 1428 zilikuwa halali, na 3 zilitangazwa kuharibika.

Rais na Mwenyekiti wa Chama cha AK Party Recep Tayyip Erdoğan, alichaguliwa tena kama Mwenyekiti wa Chama kwa kupata kura zote 1428 halali.

Uamuzi wa Bodi Kuu ya Wakurugenzi wa chama hicho, inayojumuisha wanachama 75, pia ilibainishwa kwa mchakato huo huo wa kura.

Erdoğan alitoa hotuba ya shukrani na kusema,

"Ningependa kumshukuru kila mmoja wenu kwa kuniona nastahili nafasi ya mwenyekiti kwa mara nyingine tena."

Rais Erdoğan aliongezea kusema,

"Ushirikiano wa Jamhuri (ulioanzishwa na Chama cha Harakati ya Kitaifa (MHP)) sio muungano juu ya meza pekee, bali ni muungano wa makubaliano ya mioyo."Habari Zinazohusiana