Virusi vya corona Uturuki

Watu 68 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na virusi vya corona

1595579
Virusi vya corona Uturuki

Watu 68 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na virusi vya corona (covid-19) ndani ya masaa 24 nchini Uturuki.

Idadi ya watu waliofariki kwa virusi vya corona (covid-19) tangu kuzuka kwa janga hilo hadi kufikia sasa nchini Uturuki imefikia 28,839.

Jumla ya watu 137,885 waliweza kufanyiwa vipimo vya covid-19 ndani ya siku moja ambapo kesi 685 ziligundulika. Idadi ya kesi za maambukizi ndani ya siku moja imefikia 11,322.

Idadi ya waliopona imefikia 2,601,137 ikiwa ni pamoja na watu 7,837 walioruhusiwa kuondoka hospitali.Habari Zinazohusiana