Operesheni dhidi ya PKK
Mapambano dhidi ya PKK
1594170

Vikosi vya usalama ya Uturuki, ambavyo vinaendelea na shughuli dhidi ya kundi la kigaidi la PKK licha ya hali mbaya ya hewa, vimeendelea kuwashambulia magaidi wa kundi hilo.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Uturuki, magaidi 126 wa PKK na YPG waliangamzwa katika operesheni iliyoendeshwa mwezi Februari.
Kwa upande mwingine, idadi ya wanachama wa kundi la kigaidi la kujitenga PKK / KCK, ambao walijisalimisha wenyewe mnamo 2021, iliongezeka hadi 31 kufikia Februari 27.
Operesheni za "Eren", ambazo zilianzishwa na Wizara ya Mambo ya Ndani mnamo Januari, pia zinaendelea.
Katika muktadha huu, operesheni mpya zilizinduliwa huko Bitlis, Siirt, Tunceli, Hatay, Osmaniye, Gaziantep, Hakkari na Şırnak mnamo Februari.