Ujumbe wa rambirambi wa Çavuşoğlu kwa Italia

Waziri Mevlüt Çavuşoğlu atuma ujumbe wa rambirambi kufuatia kifo cha balozi wa Italia kilichotokea nchini DRC

1589209
Ujumbe wa rambirambi wa Çavuşoğlu kwa Italia

Waziri wa Mambo ya nje Mevlüt Çavuşoğlu alituma ujumbe wa rambirambi kufuatia mashambulizi ya msafara wa Umoja wa Mataifa (UN) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo balozi wa Italia katika nchi hiyo, Luca Attanasio, alifariki.

Mevlüt Çavuşoğlu alichapisha ujumbe wa rambirambi kwenye akaunti yake ya Twitter kwa kumtambulisha mwenzake wa Italia, Luigi Di Maio.

Katika ujumbe wake kuhusu shambulizi hilo, waziri Çavuşoğlu alisema,

"Nimesikitishwa sana na kushtushwa na kifo cha Balozi wa Italia Luca Attanasio na mwanajeshi wa Italia (Carabinieri) kilichotokea kwenye mashambulizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ninatoa pole zangu za dhati kwa rafiki zangu wa Italia, familia zinazoomboleza na taifa zima la Italia kwa ujumla."

Kulingana na ripoti kwenye vyombo vya habari vya Italia, kundi la magaidi lilitumia silaha kutekeleza mashambulizi dhidi ya msafara wa Shirika la Mpango wa Chakula Ulimwenguni (WFP) mwendo wa saa 10:00 kwenye barabara kati ya miji ya Goma na Bukavu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Katika mashambulizi hayo, watu 3 walipoteza maisha: Luca Attanasio, 43 ambaye ni balozi wa Italia kwa KDC tangu 2017, mlinda usalama Vittorio Iacovacci na dereva wa WFP.Habari Zinazohusiana