Erdoğan azungumza na Putin

Rais Recep Tayyip Erdoğan amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

1586333
Erdoğan azungumza na Putin

Rais Recep Tayyip Erdoğan amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Ofisi ya Rais, mazungumzo yaligusia Uhusiano wa Uturuki na Urusi na masuala ya kikanda.

Wakati wa mkutano huo, Rais Erdoğan almesema kuwa wataalam wa Uturuki na Urusi wanaweza kuja pamoja na wenzao wa Azerbaijan ili kutengeneza njia za usafirishaji wa barabara na reli huko Nagorno-Karabakh, ambazo zinaanzishwa tena kufuatia Mkataba wa 11 Januari.

Akisema kwamba Kituo cha Pamoja huko Aghdam kimefanikiwa kutimiza jukumu la kufuatilia na kudhibiti usitishaji wa vita, Rais Erdoğan aliongeza kwa kusema kuwa juhudi za pamoja zinapaswa kufanywa katika mambo yote kulinda usitishaji vita.

Akisisitiza kuwa ni masilahi ya pamoja kutatua suala la Syria haraka iwezekanavyo, Erdoğan aliangazia ukweli kwamba fursa ya amani na utulivu nchini Libya haipaswi kupotea.Habari Zinazohusiana