Virusi vya Corona Uturuki

Watu 149 wapoteza maisha kutokana na virusi vya corona (covid-19) ndani ya masaa 24 nchini Uturuki

1569430
Virusi vya Corona Uturuki

Watu 149  wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na virusi vya corona (covid-19) ndani ya masaa 24 nchini Uturuki.

Idadi ya watu waliofariki kwa virusi vya corona (covid-19) tangu kuzuka kwa janga hilo hadi kufikia sasa nchini Uturuki imefikia 24,789.

Jumla ya watu 163,142 waliweza kufanyiwa vipimo vya covid-19 ndani ya siku moja ambapo kesi 734 ziligundulika. Idadi ya kesi za maambukizi ndani ya siku moja imefikia 5,967.

Idadi ya waliopona imefikia 2,296,050 ikiwa ni pamoja na watu 6,018 walioruhusiwa kuondoka hospitali.

Rais Recep Tayyip Erdoğan alisema licha ya janga la ugonjwa wa corona (Covid-19) kuleta shida na ugumu wa kimaisha, pia limeweza kufungua fursa mpya katika ulimwengu wa biashara.Habari Zinazohusiana