Ziara ya Çavuşoğlu nchini Pakistan

Waziri wa Mambo ya Nje Mevlüt Çavuşoğlu atekeleza ziara rasmi ya Islamabad nchini Pakistan

1562866
Ziara ya Çavuşoğlu nchini Pakistan
cavusoglu-mahmud tmv pakistan.jpg

Waziri wa Mambo ya Nje Mevlüt Çavuşoğlu amesafiri katika mji mkuu wa Islamabad nchini Pakistan kama sehemu ya ziara rasmi ya siku mbili.

Çavuşoğlu alipokewa na kukaribishwa kwanza na Rais wa Pakistan Arif Alwi.

Alwi aliwasilisha medali ya "Hilal-i Pakistan" kwa Çavuşoğlu kwenye hafla iliyofanyika Jinnah Hall.

Mevlüt Çavuşoğlu alitoa maelezo kuhusu mkutano huo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii na kusema,

"Tulifikisha salamu na matakwa mema ya Rais wetu @RTErdogan kwa Rais Alwi. Pakistan ni makazi yetu ya pili. Tutaendeleza uhusiano wetu mzuri. Najivunia kubeba nishani hii ya Hilal-i Pakistan. Tudumishe undugu kati ya Uturuki na Pakistan."

Çavuşoğlu baadaye alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Shah Mahmud Qureshi.

Mawaziri hao walijadili masuala ya uhusiano wa pande mbili, wa kikanda na wa kimataifa katika mkutano wao.

Nchi hizo mbili zilikubaliana kufuata mkakati wa pamoja wa masilahi ya pande zote katika maswala ya kimataifa ili kuboresha uhusiano.

Mawaziri hao wawili pia walielezea hofu yao juu ya kuongezeka kwa Islamophobia katika ulimwengu na kusisitiza juhudi za pamoja za kulinda maadili ya Kiislamu.

Wakati wa mkutano huo, Mkakati wa Uchumi wa Uturuki na Pakistan ulizungumziwa kwa kina.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Qureshi, aliishukuru Uturuki kwa kuunga mkono suala la Kashmir.

Baada ya mkutano wa mawaziri, mkutano kati ya wajumbe ulianza.

Hati ya makubaliano ilitiwa saini kati ya Çavuşoğlu na Wakfu wa Elimu wa Uturuki (TMV) pamoja na Waziri wa Elimu wa Pakistan Mahmoud baada ya mkutano.Habari Zinazohusiana