Mazungumzo ya Çavuşoğlu na mawaziri wa Maldives na Chad

Mevlüt Çavuşoğlu ahudhuria mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu

1535576
Mazungumzo ya Çavuşoğlu na mawaziri wa Maldives na Chad

Waziri wa Mambo ya Nje Mevlüt Çavuşoğlu, alikutana na mawaziri wenzie wa Maldives na Chad katika mji mkuu wa Niamey nchini Niger, alipokuwa amekwenda kuhudhuria mkutano wa 47 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

Kulingana na taarifa za vyanzo vya kidiplomasia, iliarifiwa kuwa Çavuşoğlu alielekea mjini Niamey, nchini Niger ili kuhudhuria mkutano wa 47 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC .

Waziri Çavuşoğlu alipokewa na kukaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger Kalla Ankourao katika uwanja wa ndege.

Çavuşoğlu baadaye alifanya mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Amine Abba Sidick na Waziri wa Mambo ya Nje wa Maldives Abdullah Shahid.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Çavuşoğlu alizungumzia mkutano wake alioufanya na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Sidick na kusema,

"Tulijadili suala la uchaguzi wa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu. Tutaendeleza msaada wetu wa elimu na maendeleo kwa ndugu zetu wa Chad."

Çavuşoğlu pia alitangaza kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Maldives Shahid na kusema,

"Tutakuza ushirikiano wetu haswa katika nyanja za uchumi, biashara, kilimo na elimu. Safari za ndege za kuelekea Male zilizozinduliwa na Shirika la Ndege la Kituruki, zitachangia pakubwa ukuaji wa sekta ya utalii kati ya nchi zetu."Habari Zinazohusiana