Virusi vya corona Uturuki

Watu 72 wapoteza maisha kwa corona ndani ya masaa 24 nchini Uturuki

1515746
Virusi vya corona Uturuki

Watu 72 wameripotiwa kupoteza maisha ndani ya masaa 24 kutokana na virusi vya corona (covid-19) nchini Uturuki.

Idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya corona imeripotiwa kufikia 9,799 nchini Uturuki tangu kuanza kwa janga la covid-19.

Jumla ya watu 112,215 wameweza kufanyiwa vipimo  vya covid-19 ndani ya siku moja ambapo kesi 2,017 mpya za maambukizi ya corona zimegundulika.

Idadi ya watu waliopona hadi kufikia sasa imefikia 314,390 ikiwa ni pamoja na watu 1,297 walioruhusiwa kuondoka hospitali.Habari Zinazohusiana