Majibu ya Rais Erdoğan kwa kiongozi wa Ufaransa

Rais Erdoğan amjibu na kumkosoa rais wa Ufaransa Macron kuhusu suala la harakati dhidi ya Uislamu

1515268
Majibu ya Rais Erdoğan kwa kiongozi wa Ufaransa

Rais Recep Tayyip Erdoğan amemkosoa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu suala la harakati dhidi ya Uislamu.

Akihutubia kwenye Mkutano Mkuu wa 7 wa Baraza la Chama cha Maendeleo na Haki uliofanyika Kayseri, Erdoğan aliuliza,

‘‘Macron ana matatizo gani na Uislamu, ana matatizo gani na Waislamu ?’’

Rais Erdoğan alimjibu na kumkosoa kiongozi wa Ufaransa kwa kusema,

‘‘Macron anahitaji kupewa matibabu ya kiakili. Mtu asiyeelewa uhuru wa kiimani, uhuru w akidini, anawezaje kuwa kiongozi wa taifa lenye mamilioni ya wananchi waliokuwa na imani tofauti z akidini. Ni muhimu kutazamwa akili yake kwanza. Halafu mtu huyo huyo anajihangaisha na Erdoğan. Kujihangaisha na Erdoğan hakuna manufaa yoyote kwako. Kuna uchaguzi unakuja baada ya mwaka mmoja. Tutaona hatima yako kwenye uchaguzi. Sidhani kama bado unayo safari ndefu. Kwanini? Kwa sababu kama hujanufaisha Ufaransa, utawezaje kujinufaisha wewe mwenyewe.’’Habari Zinazohusiana